Loading...

Aunt Ezekiel Atoboa Kuhusu Wasanii wa Bongo Movies Kujitengenezea ‘Skendo’


 

Staa mrembo wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel ‘Mama Kijacho’ amesema baadhi ya wasanii wa bongo movies hawajitambui ndio maana kazi zao nyingi hazina mvuto badala yake nguvu nyingi wameelekeza kubuni skendo wakitarajia ndio ziatawatoa kisanaa.
Alisema wasanii wengi wanatumia muda mwingi kutafakari jinsi ya kutengeneza skendo ili watume kwenye mitandao na kuandikwa kwenye magazeti lakini hawana ubunifu wa kutengeneza filamu zenye ushawishi kwenye jamii.
Aunt ambae kwenye filamu ya Chozi la Wanjaa amecheza kama mke wa Dude alisema kwamba endapo wasanii wanaofanya mchezo huo hawata badilika ni ukweli usiopingika kwamba soko la filamu inchni litaendelea kudumaa kama ilivyo sasa.
“Ni ukweli kwamba baadhi ya wasanii wa filamu hawajitambui kwani akili yao wameelekeza kwenye kutengeneza skendo badala ya kubuni namna ya kuigiza filamu ambazo zinaweza kuwa na mvuto kwenye jamiiinayoziangalia kinyume na hapo tutaendelea kusaka wachawi wanaoua soko letu’- Aunt Ezekiel alilieza gazeti la Filamu
Mdau una maoni gani juu ya hoja hii ya wasanii kutengeneza skendo, je ni kweli? Msanii gani unahisi ndio kazi yake

WAANDISHI WA HABARI RUVUMA WAPIGWA MSASA JUU YA UZURI NA UBAYA WA UCHIMBAJI MADINI YA URANI

Asasi 3 zisizo za kiserikali leo zimetoa elimu kwa waandishi wa habari mkoani Ruvuma juu ya uelewa wa uchimbaji wa madini ya urani. Asasi hizo ni Caritas, MVIWATA Ruvuma na TMMTF.


Elimu iliyotolewa kwa waandishi hao wa habari ni kuimarisha elimu ya ushawishi kwa jamii katika faida na madhara ya madini ya urani, pia utafiti wa kisayansi ili kuainisha faida na madhara ya urani kwa binadamu na mazingira.


Katika semina hiyo uchimbaji wa madini umeonekana kuwa na madhara zaidi kuliko faidi kwa Watanzania. Habari zaidi itawajia muda mfupi.

Mr. Martine kutoka Ujerumani ni mmoja kati ya watoa mada



Mr. Martine na Mr. Mahundi wakujadiliana



Mr. Mahundi akitoa mada juu ya uandishi wa habari za kiuchunguzi



Ally Mzava kutoka CESOPE Dodoma akitoa mada juu ya uzoefu wa kuelimisha wananchi kuhusu athari za madini ya urani



Mr. Jeremia Araka mhadhiri wa chuo kikuu AJUCO akitoa mada juu ya misingi na maadili ya uandishi bora wa habari



Mr. Brito Mgaya akiwasilisha moja ya mada juu ya athari za madini ya urani



Mwandishi wa habari wa RFA Ngahyona Nkondora akiuliza swali kwa watoa mada


Joyce Kalinga mwakilishi wa TMMTF


Mwambije mwandishi wa habari wa ITV


Nathan Mtega - ITV


Gideon Mwakanosya - NIPASHE


Tamimu Gillo - Radio Jogoo Songea


Geofrey Nilai - Radio Maria



Waandishi wa Habari wakimfuatilia kwa makini mtoa mada


Mr. Yazidu Athuman mkazi wa Namtumbo jirani na mgodi wa urani akielezea kwa uchungu athari walizoanza kupata kabla uchimbaji haujaanza



Waalamu wa asasi zilizoandaa semina kwa waandishi wa habari wakifanya tathimini ya semina



Waandishi wa habari wakifanya tathimini ya semina

KIONGOZI WA WASABATO DUNIANI AJA TANZANIA


 
Kiongozi wa Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA) duniani, Askofu Ted Wilson anatarajiwa kuwasili nchini leo kwa ziara ya kikanisa ya siku nne. 
Taarifa iliyotolewa na kanisa hilo, jijini Dar es Salaam, inaonesha kuwa kiongozi huyo anakuja nchini kushiriki Sherehe za Utume zilizoandaliwa na kanisa hilo na kujumuisha nchi zingine 11 za Afrika Mashariki na Kati.
Pamoja na kushiriki kwenye sherehe hizo, lakini kiongozi huyo atashiriki kwenye kuzindua miradi mbalimbali ya afya na elimu ya kanisa hilo nchini.
Sherehe hizo ambazo zinatarajiwa kuvuta zaidi ya watu 50,000 kutoka nchi hizo 11 na sehemu zingine duniani, zitakwenda sambamba na utoaji wa huduma mbalimbali za kijamii, ikiwa ni pamoja kupima afya kwa magonjwa mbalimbali kama ya moyo, sukari, Ukimwi na magonjwa mengine.
Juzi Kiongozi wa Mawasiliano wa kanisa hilo katika ukanda wa Kati na Mashariki mwa Afrika, Mchungaji Steven Bina alisema mkutano huo wa siku nne, ambao unafanyika Uwanja wa Taifa ni wa aina yake na wa kwanza kufanyika nchini.
Katika mfululizo wa sherehe hizo, jana kulizinduliwa ujenzi wa Makao Makuu ya Jimbo la Kusini Mashariki mwa Tanzania (SEC), ambayo yatajengwa katika maeneo ya Kwembe, nje kidogo ya Dar es Salaam.
Shughuli zingine ambazo zilifanyika juzi ni uzinduzi wa kituo cha vitabu, ambacho kipo eneo la Ilala na kitatoa huduma kwa wakazi wa Dar es Salaam, ambao watahitaji vitabu mbalimbali vikiwemo vya afya na aina vya vyakula vinavyofaa kwa mwili wa binadamu. Kituo hicho kilizinduliwa na Mkurugenzi wa Idara ya Uchapishaji ya kanisa hilo duniani, Mchungaji Howard Faigao.
Miongoni mwa shughuli zingine ambazo zitafanywa na kanisa leo ni utoaji wa vitabu 1,000 na jozi 300 za viatu kwa ajili ya shule za msingi, na utoaji wa vifaa vya maabara kwa ajili ya shule za sekondari. Vitu hivyo vitatolewa kwa manispaa ya Ilala, ambayo ndio itakayovisambaza mahali ambako kuna mahitaji.
Mkutano huo unahusisha washiriki kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Rwanda, Burundi, Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Eritrea, Somali, Ethiopia, Sudan Kusini na Djibout. Baadhi ya kwaya pia zitatoka nje ya Bara la Afrika.
Tamasha hilo kubwa la kitume, linatarajiwa kuhutubiwa kesho na Rais Jakaya Kikwete. Lakini pia kutakuwepo na viongozi wengine wapatao 400 wa kanisa hilo kutoka ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Sherehe hizo zenye kauli mbiu ya “Kusherehekea Mibaraka ya Mungu katika Utume”, zinafanywa na kanisa hilo ikiwa ni njia ya kujivunia mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika upelekaji wa injili na utoaji wa huduma za jamii.

AFISA ELIMU MBINGA AVULIWA MADARAKA


BARAZA la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma limemvua madaraka afisa elimu msingi wa wilaya hiyo Daniel Mkali baada ya kufanyiwa uchunguzi kwa muda kwa tuhuma mbalimbali zilizotajwa na baadhi ya madiwani pamoja na viongozi wa idara hiyo ya elimu msingi na kuelekea kutishia kuibuka kwa mgogoro wilayani humo.

Akitangaza uamuzi huo wa kumvua wadhifa huo pamoja na kumshusha cheo na kutakiwa kupangiwa shule ya kufundisha mwenyekiti wa halmashauri hiyo ya Mbinga Alanus Ngahi, mbele ya madiwani pamoja na watumishi wengine wa halmashauri hiyo amesema uamuzi huo umefikiwa na kamati ya maadili iliyokutana kujadili suala hilo la kinidhamu na kiutumishi na baraza hilo kuridhia hatua zichukuliwe dhidi ya afisa elimu huyo.

Akizitaja tuhuma nne zilizokuwa zikimkabili afisa elimu huyo, mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga Hussein Isa amesema ni pamoja na kusajili asasi isiyokuwa ya kiserikali iliyojulikana kwa jina la (UWEKAMBI) umoja wa waratibu elimu kata ya Mbinga na kuwaagiza walimu wakuu wa shule za msingi wilayani humo kuhamishia fedha zote za capitation na michango ya Umitashumta jumla ya shilingi milioni 232 ambapo katika fedha hizo shilingi milioni 60 ni michango ya Umitashumta, milioni 10 ni michango ya wazazi na shilingi milioni 61 ni fedha kwa ajili ya capitation na mitihani zilipelekwa kwenye akaunti yenye namba 61714000405 iliyopo katika benki ya NMB tawi la Mbinga.



Ameitaja tuhuma nyingine kuwa ni kughushi nyaraka kwa lengo la kutoa fedha kupitia ununuzi wa mafuta ya diesel lita 5500 na petrol lita 5500 na kuwaagiza walimu wakuu wachangie fedha za kupiga picha wanafunzi wa darasa la saba pamoja na fedha kwa ajili ya TSM 9 kwa maelekezo hayo ni kosa kwa sababu alikuwa akijua kuwa gharama za TSM 9 hugharamiwa na serikali kwa asilimia mia moja.

Amesema kati ya fedha hizo kiasi cha shilingi milioni 12.47 zilipelekwa kwenye akaunti hiyo ya UWEKAMBI na ameitaja tuhuma nyingine kuwa ni kumdanganya mwajiri kuwa hakujakusanywa fedha yoyote kutoka kwa wazazi na hakuna fedha ya capitation iliyopelekwa kwenye akaunti hiyo ya UWEKAMBI.

Aidha mkurugenzi mtendaji amesema baada ya maamuzi hayo yaliyotolewa na baraza la madiwani hatua nyingine zinazohusishwa na mamlaka nyingine zikiwemo za kinidhamu zitafuata ingawa kwa sasa anapaswa kuyatumikia maamuzi yaliyotolewa na baraza hilo la madiwani.

CHENGE AGEUKA MBOGO BUNGENI BAADA YA KUITWA FISADI...AMTAKA HALIMA MDEE ATOE USHAHIDI KUTHIBITISHA KAULI YAKE


MBUNGE wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) ametakiwa kuwasilisha ushahidi kuthibitisha kauli yake ya kumtuhumu Mbunge Bariadi Magharibi, Andrew Chenge (CCM), kwa ufisadi.

Chenge alilazimika kuomba utaratibu wa kiti juzi, baada ya Mbunge huyo wa Kawe kumtaja mara mbili wakati akichangia mjadala wa taarifa za kudumu za Bunge zilizowasilishwa juzi.




Mara ya kwanza, Mdee alimhusisha Chenge na mkataba mbovu wa Kampuni ya Ndege (ATCL) uliosababisha Serikali kuingia hasara ya zaidi ya Sh bilioni 90.

Licha ya kumtaja kwenye ufisadi huo ambao kwa mujibu wa Mdee, Chenge ndiye alikuwa Waziri wa Wizara yenye dhamana na ATCL, pia alimtaja kuhusika katika kashfa nyinginezo ikiwemo suala la utoaji takribani Sh bilioni 200, katika iliyokuwa Akaunti ya Tegeta Escrow ya Benki Kuu (BoT).

“Wabunge tuanze kuchunguzana humu ndani na kushughulikiana,” alisema Mdee na kutaja kwamba kwa kuanza, waanze na Chenge pamoja na Dk Shukuru Kawambwa (Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi), akimhusisha kuwa aliwahi kushika wizara hiyo yenye dhamana na ATCL.

Kauli hiyo ilimfanya Chenge kusimama na kusema; “kwa heshima zote nimemvumilia sana mheshimiwa (Mdee) anayechangia hoja hii. Kama ana ushahidi wa hayo anayosema, kanuni zetu zinatutaka ayawasilishe mbele yako.

“Mimi ningelipenda Bunge hili liendelee kuwa na heshima yake. Pili naomba sana, hayo wanayoyasema wawe na ujasiri wa kwenda kuyasemea nje ya ukumbi huu wa Bunge, wasijifiche kwenye kinga ya Bunge.

“Nina mengi ya kusema, lakini kwa sababu nimesimama kwa hoja ya utaratibu, kunitaja moja kwa moja, naomba aweke hoja mezani,” alisema Chenge.

Mwenyekiti wa Bunge alikubaliana kwamba Mdee awasilishe ushahidi kwa kiti. Hata hivyo Mdee alijibu, “Kuna utaratibu wa kikanuni, vielelezo nikitakiwa kuleta nitaleta.

"Tunazungumza hapa matumizi mabovu, mikataba mibovu na wizi wa mali ya umma. Mzee wangu (Chenge) ni rafiki yangu lakini nimeamua nimfungukie kwa sababu haya ni mambo makubwa.”
Older Posts
© Copyright Bongo Mirror | Designed By BONGOJAMII.COM
Back To Top