Loading...

UKATILI ULIOJE! WAZAZI WAMPIGA, WAMFUNGA KAMBA MTOTO WAO, WAMFUNGIA NDANI


Katika hali inayoonyesha ukatili wa ajabu, mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Asha Mohamed, akishirikiana na mumewe, walimfunga kamba miguu na mikono mwanaye wa kumzaa Salum Mohamed (9) na kumfungia ndani ya nyumba yake huku wenyewe wakienda kusikojulikana muda mrefu Jumatatu iliyopita huko Mkundi, nje kidogo ya mji wa Morogoro.

Polisi wakimfungua kamba mtoto huyo alizokua amefungwa na wazazi wake.

Tukio hilo la kusikitisha lilifanyika ikiwa ni adhabu ya mtoto huyo kutokana kosa la kuchana chandarua kwa miguu, kitendo alichokifanya usiku wa Jumapili, ambako licha ya kupigwa kwa zaidi ya saa mbili mfululizo, pia alinyimwa chakula na hivyo kulala na njaa.

Polisi wakiwa wamembeba mtoto huyo.

Kwa mujibu wa majirani, Asha na mumewe ambaye ni baba wa kambo wa mtoto huyo, wamekuwa na tabia ya kumtesa, kitendo ambacho awali, kiliwahi kumfanya atoroke nyumbani hapo kukimbilia mjini kwa bibi yake, umbali wa zaidi ya kilomita kumi

Mama mzazi wa mtoto huyo aliefahamika kwa jina la Asha Mohamedi.

Kwa mujibu wa majirani Mwanamke huyo na mumewe kwa muda mrefu walikuwa wakimfanyia vitendo vya kikatili mtoto huyo”kuna wakati mtoto huyu aliamua kutembea kwa kwa miguu kutoka hapa mkundi mpaka mjini kwa bibi yake umbali wa kilomita 10.

Waandishi wa habari wakifanya mahojiano na mtoto huyo baada ya kufunguliwa kamba.

“Wazazi wake jana majira ya saa 3 mpaka saa 5 usiku walimpiga sana huyu mtoto, cha ajabu asubuhi walimfunga kamba na kumfungia kwa nje na kufuli kubwa na wenyewe kwenda kwenye shughuli zao, alishindwa kwenda shule, tulipomuuliza kupitia dirishani, alisema alipewa adhabu hiyo baada ya kuchana chandarua, kwa uchungu tukaamua kutoa taarifa kwako,” alisema Mage Luzimamu, mmoja wa majirani.

Baada ya mwandishi kupata taarifa hizo aliwasiliana na Jeshi la Polisi ambapo askari walienda hadi ilipo nyumba hiyo na kulazimika kuvunja mlango na baadaye kumfungua mtoto huyo na kuondoka naye. Mama mzazi alipatikana na kukiri kuhusika na tukio hilo, ambapo alijitetea kuwa alimfunga kamba kama sehemu ya adhabu na siyo mateso.

Mume wa mama huyo alikimbia baada ya kusikia taarifa za kusakwa kwake lakini Polisi wamesema watamtafuta hadi wamtie mbaroni.

MKE ACHINJWA KISA KWENDA SALUNI



Stori: Dege Masoli, Tanga

HII ni zaidi ya ukatili! Jiji la Tanga bado linazizima kufuatia mauaji ya kutisha yanayodaiwa kufanywa na mwanaume aitwaye Khalfan Hamad (46), dhidi ya mkewe, Mary Lucas (20) kwa kumchinja na panga kisa kikidaiwa ni wivu wa mapenzi, Uwazi lina mkasa mzima.

Enzi za uhai wake, Mary Lucas (20) anaedaiwa kuchinjwa na mumewe.


Tukio hilo lililoacha simulizi ya kushangaza miongoni mwa wanandoa na wanaotarajia kuingia, lilijiri Aprili 18, mwaka huu nyumbani kwa mwanaume huyo, Mtaa wa Mapinduzi ‘A’ Kata ya Duga jijini hapa.

WANACHOKIJUA POLISI WA TANGA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, ACP Zuberi Mwombeki alitangaza kwa waandishi wa habari kwamba, mauaji hayo yalitokea saa nne na nusu asubuhi ya Aprili 18 mwaka huu.

Alisema chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi kati ya wawili hao ambapo marehemu alimuomba mumewe pesa kiasi cha shilingi elfu kumi aende saluni kutengeneza nywele lakini mwanaume akasema hana.

“Mwanaume hakumpa pesa marehemu lakini baadaye alimkuta amesuka na ndipo ugomvi ulipoanzia hapo hadi kutokea mauaji hayo,” alieleza kamanda huyo.

UWAZI LAANZA NA MAJIRANI

Mengi yamesemwa kufuatia mauaji hayo, lakini kama kawaida ya Gazeti la Uwazi ni kufuatilia kwa kina ili kujua chanzo cha kila habari inayotakiwa kuandikwa gazetini.

Ili kujua nini kilitokea kabla na baada ya mauaji hayo, Uwazi lilizungumza na baadhi ya majirani wa nyumbani kwa mtuhumiwa huyo ambaye kwa sasa anashikiliwa na polisi chini ya ulinzi mkali.

“Jamani sisi wenyewe tumeshtuka sana kwa kifo cha Mary, mimi nimeongea naye akiwa anakwenda saluni na hata aliporudi. Kama angejua ndiyo siku yake ya kufa naamini asingekwenda. Inauma sana!

“Mary alitoka saluni akiwa amependeza maana alitengenezwa nywele vizuri sana. Mimi mwenyewe nilimsifia. Kufika nyumbani kwake, mzozo ukaanza.

“Mumewe alitaka kujua alikotoa shilingi elfu kumi ya kuendea saluni maana yeye hakumpa. Mzozo ulikwenda hadi mwanaume akachukua panga na kumchinja. Naamini ni wivu,” alisema jirani mmoja.

KUMBE WALIKUWA NA HISTORIA YA UGOMVI

Jirani mwingine, Shaban Juma yeye alisema: “Hawa watu wameishi katika hali ya kutoelewana na walikuwa wakigombana kila wakati, lakini hatukujua kama litatokea hili kwani mara zote katika kugombana kwao, mwanaume ndiye aliyekuwa akipigwa jambo ambalo liliwafanya watu wa karibu yake kumshauri kuvunja uhusiano wao kulikoni aibu ya kupigwa na mke.”

Jennifer Charles yeye pia ni jirani, alisema: “Siku ya tukio Mary alimwomba mumewe hela ya kwenda kutengeneza nywele saluni lakini mume hakuwa na pesa siku hiyo lakini baada ya kuondoka nyumbani, marehemu naye alikwenda saluni.

“Baadaye mume aliporudi nyumbani hakumkuta Mary lakini mara alirudi akiwa ametengenezwa nywele jambo lililomfanya bwana kuhisi kuwa fedha hizo amehongwa na mwanaume mwingine tofauti na yeye na hivyo kuzuka ugomvi huo.”

MUME ALITOKA NJE AKITAMBA KUUA

Baada ya Jennifer kumaliza kusimulia hayo, Juma Ally, naye ni jirani, akaendeleza: “Hatukujua kilichoendelea katika mzozo wao, lakini baadaye ukimya ulitawala. Muda mfupi mbele mume alitoka nje na kutuambia kwamba ameshaua huko ndani kwani amechoka kupigwa na sasa amejibu mapigo.

“Kwanza tulijua anatutania lakini tulivyoona kimya kimezidi tukaamua kuingia ndipo

tulipomkuta marehemu akiwa chini, akitoka damu nyingi. Tuliogopa kwa kweli. Mary mrembo tunayemjua sisi, amelala chini na damu chapachapa.

“Alikuwa ana majeraha makubwa sehemu ya shingo na kichwani yaliyotokana na kupigwa na panga. Ilionekana panga lilikuwa kali sana na panga lenyewe lilikuwa pembeni yake. Ndipo tulipoamua kumkimbiza Hospitali ya Mkoa, Bombo ambapo alipoteza maisha wakati madaktari wakihangaika kuokoa uhai wake.”

ASINGEKUFA MKE

Naye, Fatuma Ramadhani alisema kutokana na ugomvi wa mara kwa mara kati ya wawili hao na mwanaume kupigwa kila wakati, majirani waliamini siku moja mume huyo ndiye angekuja kupata madhara hata kufa kutokana na alivyokuwa akipigwa.

MTUHUMIWA KUPANDA MAHAKAMANI WAKATI WOWOTE

Kamanda Mwombeki alisema upelelezi unaendelea ili kuweza kumfikisha mahakamani mtuhumiwa huyo. Marehemu Mary alizikwa katika eneo la Mwakizaro jijini Tanga, siku ya pili baada ya tukio hilo la kuhuzunisha

MAMA KANUMBA, MAMA LULU KIMENUKA!




Mwandishi wetu
Taarifa zilizotua kwenye dawati la gazeti hili zinadai kuwa, wale wamama wa mjini ambao walikuwa mashosti hadi kufikia hatua ya kusema ni kama ndugu, mama wa aliyekuwa staa wa Bongo Movies, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa na mama wa mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’, Lucresia Karugila, sasa kimenuka!

Mama wa mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’, Lucresia Karugila.

DALILI KUWA PAKA NA CHUI
Chanzo chetu cha kuaminika kilidai kuwa, dalili za wawili hao kuelekea kugeuka kuwa paka na chui zilianza muda mrefu lakini hali ikazidi kuwa mbaya Siku ya Kumbukumbu ya Kifo cha Kanumba, Aprili 7, mwaka huu alipokuwa akitimiza miaka mitatu kaburini.

CHANZO NI LULU
Ubuyu ulidai kwamba, siku ya kumbukumbu ya kifo cha Kunumba, Mama Kanumba alimtuhumu Lulu kutotoa ushirikiano na kufikia hatua ya kutoa maneno makali zaidi yaliyomkera mama Lulu.



Mama wa aliyekuwa staa wa Bongo Movies, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa.

MAMA KANUMBA NA SMS MBAYA KWA MAMA LULU
Ilidaiwa kwamba, siku ya kumbukumbu ya kifo cha Kanumba, mama Kanumba alimtumia mama lulu sms mbaya ya kejeli (kuiandika hapa siyo busara) ndipo mama Lulu ‘alipofyumu’ na kuona kwa hali hiyo bora kama mbwai na iwe mbwai.“Ile sms mama Kanumba alimtumia mama Lulu siku ile (Aprili 7) majira ya saa 11:00 alfajiri.

HAIKUWA YA KIUNGWANA
“Kwa kweli ilikuwa meseji mbaya mno. Alikuwa akimuagiza mama Lulu amuamshe Lulu kwa ajili ya kwenda kaburini kwa Kanumba lakini haikuwa ya kiungwana.“Hata hivyo, ukweli mama Lulu alitumia busara kwa kutomjibu lakini akadhamiria kuchukua hatua za kisheria,” alidai mtoa ‘ubuyu’ huyo.Enzi za ushosti wao.

Ilizidi kudaiwa kwamba, wakati mama Lulu akitafakari sababu ya shosti wake huyo ambaye walikuwa wakitembea mjini kama kumbikumbi kumtumia sms hiyo, akashangaa kusoma tena kwenye gazeti mama Kanumba akimpa vipande vyake Lulu, jambo lililozidi kumchefua mama Lulu.

KUBURUZANA KORTINI?
“Kimsingi hali ni mbaya sana sasa hivi, inavyoonekana mama Lulu kamchoka mama Kanumba na anataka kuchukua hatua zaidi ikiwemo kuburuzana kortini,” alidai sosi huyo.

MAMA LULU AFUNGUKA
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, gazeti hili lilimtafuta mama Lulu ambapo alipopatikana alikiri kupokea ujumbe na kwamba hali ni mbaya sana.“Nimeumizwa sana na sms ya mama Kanumba lakini siwezi kuwapa kwa sababu nataka kuifanyia kazi,” alisema mama Lulu.

Mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’.

MAMA KANUMBA VIPI?
Kwa upande wake mama Kanumba aliendelea kusisitiza kuwa yeye ataendelea kumlilia mwanaye na hana mpango na familia hiyo ya Lulu.“Mimi kwa upande wangu nitamlilia mtoto wangu mpaka siku ya kufa kwangu lakini kinachoniuma ni Lulu kufanya sherehe ya mdogo wake siku ya kumbukumbu ya mwanangu.

“Jamani hata kama mtu ana roho gani, hawezi kufanya hivyo,” alisema.
Alipoulizwa kuhusu sms aliyomtumia mama Lulu na kwamba mama huyo yupo mbioni kumchukulia hatua za kisheria hakuwa tayari kuzungumza chochote.

P-SQUARE KUMZIKA BABA YAO KESHO IJUMAA BAADA YA KUFARIKI MIEZI MIWILI ILIYOPITA!



Mzee Moses Okoye na mtoto wake Peter wa P Square. Hii ilikuwa siku ya harusi ya Peter.



November 26, 2014 taarifa kubwa kutoka Nigeria ilikuwa ni taarifa ya msiba wa mzee Moses Okoye, baba mzazi wa mastaa wa muziki kutoka Nigeria, P Square.



Tangu mzee huyo afariki ni miezi miwili sasa, yamepita matukio mengi huenda tukawa tumeanza kusahau tukio hilo, story iliyoko mitandaoni kutoka Nigeria ni kuhusu ndugu pamoja na familia ya mzee huyo kuandaa mazishi yake.

Tarehe ambayo imepangwa kufanyika mazishi hayo ni January 30, ambayo ni kesho siku ya Ijumaa.
Older Posts
© Copyright Bongo Mirror | Designed By BONGOJAMII.COM
Back To Top