Loading...

PICHA ZOTE ZA MAZISHI YA BRIGEDIA JENERALI MBITA, JK AMLILIA


 

Mwili wa Brigedia Jenerali Hashim Mbita ukiswaliwa Msikitini.

Mwili wa Marehemu Mbita ukiingizwa kwenye gari maalum la Jeshi kwa ajili ya kupelekwa makaburi ya Kisutu Dar kwa maziko.

Safari ya kuelekea makaburini kwa ajili ya maziko ya Mbita.

Rais Mstaafu wa awamu ya tatu wa Tanzania, Benjamin William Mkapa akiwa katika jukwaa lililokuwa limeandaliwa katika Makaburi ya Kisutu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (wa nne kushoto) akiwa katika jukwaa lililoandaliwa katika makaburi ya Kisutu.

Brasbendi ya JWTZ ikiongoza maandamano ya waombolezaji katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

Majenerari wastaafu (kushoto) wakiongozwa na Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Samweli Ndomba aliyevaa kombati wa tatu kulia.

Maafisa wa JWTZ wa vyeo vya Meja wakipeleka mwili wa Marehemu Brigedia Mbita Kaburini.

Wanajeshi wa JWTZ wakiwa kwenye paredi maalum la mazishi ya Brigedi Mbita katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam jana.

Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Ulinzi na Usalama Dkt. Jakaya Kikwete akitoka kuweka udongo kwenye kaburi la Marehemu Brigedia Mbita kama inavyoonekana pichani.

HATIMAYE mamia ya wananchi wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete jana walijitokeza kumzika aliyekuwa Katibu wa Kamati ya Ukombozi kwa nchi za Kusini mwa Afrika, Brigedia Jenereli Mstaafu Hashim Mbita.

Kabla ya kuzikwa kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam, mwili wa marehemu Mbita ulifikishwa katika msikiti wa Kwa Mtoro Kariakoo kwa swala maalum ya mazishi.

Marehemu Brigedia Jenerali Hashim Mbita alizaliwa Novemba 2, 1933 katika kijiji cha Songoro, mkoani Tabora. Katika utumishi wake alishika nyadhifa mbalimbali, ikiwemo Ofisa Habari Mkuu wa Serikali mwaka 1962 hadi 1965 na mwandishi wa habari wa rais 1965 hadi 1967.

Marehemu Mbita pia enzi za uhai wake aliwahi kuwa Mwalimu wa siasa katika Chuo cha Kijeshi cha Monduli mwaka 1969 hadi 1970, Katibu wa Kamati ya Ukombozi Kusini mwa Afrika, 1972 hadi 1989 na Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe kuanzia 2003 hadi 2006. Brigedia Jenerali Hashim Mbita alifariki dunia Aprili 26 mwaka huu katika hospitali ya Jeshi ya Lugalo na alizikwa jana katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam

SOMA HII,, DIAMOND PLATINUMZ, ZARI NDANI YA POWER BREAKFAST NA CLOUDS 360 KESHO





HOT NEWS,,UNENE WAMTESA SELENA GOMEZ






Staa wa muziki wa Pop, Selena Gomez.

NEW YORK, MAREKANI

WAZUNGU bwana! Staa wa muzikiwa Pop, Selena Gomez ameendelea kuteswa na unene ulioongezeka kwa muda mfupi huku mitandao ya kijamii ikimshambulia. Staa huyo aliyekuwa mpenzi wa staa mwenzake wa muziki, Justin Bieber kupitia ukurasa wake wa Instagram, mashabiki wake wengi wameonekana kukerwa na unene huo jambo linalomnyima usingizi staa huyo.



Kabla hajaongezeka unene.

“Selena anachukizwa na watu wanaoongelea unene wake na hilo linamuweka katika wakati mgumu wa kumsikia kila mtu akimuongelea, anaumia sana,” alisema shabiki mmoja wa staa huyo.

UNAPOMSIFU MPEZI WAKO KWA UJUZI WAKE, HUJIULIZI KAUTOA WAPI..!!






Kwetu tunaamini mchawi aliyekubuhu, ni yule aliyeuwa watu wengi zaidi. Au hata ukimuona dereva anakimbiza gari barabarani unaamini ana uzoefu wa udereva wa mda mrefu na atakuwa ameshawahi kuendesha magari mbali mbali.

Sasa linapokuja swala la mahusiano, ninaona watu wanalalamika kuhusu ujuzi wa wenzi wao. Ingekuwa mimi, endapo mwenzi wangu angekuwa na kiwango kidogo cha ujuzi kwenye maswala ya chumbani, lingekuwa jambo la furaha na kheri.
Pale unapotaka mpenzi wako awe na ujuzi wa PhD katika maswala ya chumbani, wewe unataka awe amejifunzia wapi? Kama unataka mjuzi, nenda kachukue Changu doa ambaye anajua michezo yote...
Dada zetu waliofunzwa wakatulia, na kaka zetu au wadogo zetu waliofunzwa wakatulia technically watakuwa na ujuzi mdogo na over the time katika maisha yao ya mahusiano (ndoa) wataweza kujifunza na kuimprove.

Ukimpata yule anayekupeleka puta, inabidi ukae chini na ujiulize atakuwa amewapitia au amepitiwa na wangapi mpaka akapata utaaalam huo?

BARUA NZITO: WASTARA AOMBA RADHI‭, WAMUONYA KU‬BADILI MWELELEKEO !‬




Wastara Juma

KWAKO mwanamke unayejua kuuvaa vyema uhusika katika sinema za Kibongo, Wastara Juma. Za siku nyingi? Uko poa mama!&ke?

Ukitaka kujua afya yangu mimi ni mzima wa afya, naendelea na mishemishe zangu za kila siku kuhakikisha mkono unakwenda kinywani. Nimekukumbuka hapa leo maana ni kitambo kidogo hatujaonana. Nikaona ni vizuri kukuandikia barua.

Dhumuni la barua hii ni kwanza kutaka kukukumbusha juu ya heshima niliyokuwa nakupa. Nilikuwa nakuheshimu kama mama wa watoto wawili, mtu mzima mwenye busara za kutosha.

Kwa levo ya heshima niliyokuwa nakupa, sikuwahi kuwa na shaka kwamba labda kuna siku unaweza ukabadilika. Niliamini kadiri siku zilivyozidi kusonga ndivyo busara zaidi zingeendelea kujaa katika kichwa chako.

Nilikuheshimu kama mama jasiri sana. Historia ya maisha yako inaonesha umepitia mitihani mingi, kwa namna ambavyo umepambana na kuvuka viunzi hivyo, hakuna ambaye anaweza kuwa na shaka na wewe zaidi ya kukupongeza na kukuona ni mfano wa kuigwa.

Ulipambana sana kutetea uhai wa mumeo hadi pale Mungu alipomchukua. Nikwambie Watanzania walikupa heshima ya juu. Mimi mwenyewe nilikuheshimu sana. Sikuwahi kutarajia kama siku moja unaweza kushusha heshima yako kirahisi kama wafanyavyo baadhi ya wasanii.

Sikuwahi kuwaza kama kuna siku ninaweza kukuona umevaa mavazi ya ajabu kama wafanyavyo baadhi ya wenzako, achilia mbali ulevi wa kupindukia.

Niliamini wewe ndiye mtu wa kukemea wenzako wanaotoka nje ya mstari wa kujiheshimu.

Licha ya kukuheshimu huko kwa muda mrefu, juzikati ulifanya tukio ambalo nilipoliona, akili yangu ilishindwa kuamini kama ni wewe yule ninayekuheshimu. Nazungumzia matusi mazito uliyoyaporomosha kwenye mtandao wa Instagram.

Ulimtukana mmoja wa mashabiki wako matusi mazito ya nguoni. Najua kabisa kwamba alikuudhi na kama binadamu unakasirika, lakini siku zote kabla ya kufanya jambo lolote lazima kwanza uangalie nafasi yako katika jamii.

Huwezi kumuona chizi anakutukana eti na wewe ukamtukana ili kumkomoa. Mwenye busara na hekima, akitukanwa na chizi, hukaa kimya na mwisho wa siku watu hubaini nani ni chizi!

Kwa matusi uliyomlipizia yule shabiki wako, waungwana walikujadili wewe uliyejibu badala ya shabiki wako.

Walikuona hukutumia busara. Kwa nafasi yako katika jamii, ukisema umjibu kila atakayekutukana, utawatukana wangapi? Jamii nayo itakuelewaje?

Nikuambie tu dada yangu hukufanya kitu kizuri hata kidogo, wewe ni staa mwenye heshima kubwa, huwezi kutukana matusi mazito kiasi kile hadharani, tena kwenye akaunti yako ambayo unaitumia kufanya biashara mbalimbali.

Binafsi tangu siku ile niliposoma posti yako nilijisikia vibaya, sikutegemea. Ningekushauri, ili kurejesha heshima yako, omba radhi na kubadilika. Kwa leo ni hayo tu.

Wasalaam
Newer Posts Older Posts
© Copyright Bongo Mirror | Designed By BONGOJAMII.COM
Back To Top