Loading...

FAMILIA WASHAMBULIA DIAMOND ,,,,,TUNASHAKA NA MIMBA YA ZARI



SHAKA! Familia ya ‘President’ wa Kruu ya Wasafi, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ imeamua kuweka kikao kummbana staa huyo aweke wazi kama ni kweli ana uhakika mimba aliyonayo mjasiriamali Zarinah Hassan ‘Zari’ ni ya kwake au magumashi, Risasi Mchanganyiko linakupa mchapo kamili.

Diamond Platnumz akibusu tumbo la mpenzi wake Zari.

TUJIUNGE NA CHANZO

Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na familia ya staa huyo, ndugu wa karibu akiwemo mama, binamu yake Romy Jons, wajomba zake, mameneja na marafiki wa karibu wa familia, waliamua kuweka kikao hicho usiku hivi karibuni ili Diamond athibitishe kama kweli kiumbe kinachoripotiwa kuwa ni cha kwake magazetini ni chake kweli.

Diamond akiwa katika pozi na mpenzi wake Zari.

“Ndugu walichachamaa, walitaka kujua kama kweli mimba inamhusu Diamond au ni magumashi ya kiki za vyombo vya habari.

“Kwenye hicho kikao walimualika na Diamond mwenyewe ili aweze kufunguka kama ana uhakika kweli mimba ni yake,” kilisema chanzo hicho

WALITAKA ATOE MSIMAMO

“Mbali na kutaka kujua kama mimba ni yake, walitaka pia kujua ana msimamo gani na Zari maana kila kukicha wanasikia mambo tofauti katika mitandao na vyombo vya habari,’’ kilisema chanzo hicho.

SABABU ZAZIDI KUANIKWA

Chanzo hicho kilipobanwa na mwanahabari wetu kuhusiana na sababu zilizowafanya ndugu wa Diamond watilie shaka mimba hiyo, kilisema ni kauli ambazo ziliwahi kusemwa na aliyekuwa mpenzi wake Penniel Mungilwa ‘Penny’ na aliyekuwa mume wa Zari, Ivan Semwanga.

“Walishitushwa na kauli ambayo aliwahi kuitoa Penny kwamba Diamond hana uwezo wa kumpa mwanamke mimba lakini kama hiyo haitoshi, waliitafakari kauli ya mume wa Zari ambaye alidai Zari hawezi kumzalia Diamond ndiyo maana wakataka wapate uhakika,” kilisema chanzo hicho.

MUAFAKA WA KIKAO

Chanzo hicho kikizidi kumwaga ubuyu mbele ya kinasa sauti cha Risasi Mchanganyiko kwamba, baada ya Diamond kubanwa na nduguze, alithibitisha kuwa Zari ndiyo kila kitu kwake kwa sasa, hivyo wasiwe na shaka yoyote juu ya kiumbe kinachotarajiwa kuzaliwa.

“Diamond aliwahakikishia kwamba mzigo ni wake, na msimamo wake ni kufika katika hatua ya ndoa Mungu akijalia.

KUMVISHA PETE

“Kuonesha yupo serious baada ya Diamond kuwatoa hofu ndugu zake, alisema atafanya sapraiz siku ya Mei Mosi katika shoo ya mrembo huyo, All White Party itakayofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar,” kilisema chanzo hicho na kudokeza kuwa Diamond atamvisha pete mrembo huyo.



DIAMOND AFUNGUKA

Ili kuweza kupata ukweli, mwanahabari wetu alimtafuta Diamond ili aweze kuweka wazi juu ya kikao hicho na kama ni kweli anatarajia kumvisha pete Zari. Diamond alifunguka:

“Yeah ni kweli ndugu zangu walikuwa na shaka lakini nimewahakikishia kwamba kiumbe kilichomo tumboni mwa Zari ni mali yangu, kuhusu kumvisha pete ni mapema kidogo kulizungumzia lakini watu wahudhurie kwa wingi katika shoo ya Zari White Party Ijumaa hii pale Mlimani City kwani nimeandaa sapraizi nyingi sana.

“Mei Mosi itakuwa ni siku ya kihistoria sana kwake kwani kuna mambo muhimu mengi natarajia kumfanyia mpenzi wangu Zari, watu watajua rasmi nia yangu kwa Zari maana ni mwanamke ambaye ameamua kujitoa kwa ajili yangu, hivyo sina budi kumuonesha upendo stahiki, nitafanya kila linalowezekana kumuonyesha namna gani nampenda.”

SHOO YA KIHISTORIA

Kwenye shoo hiyo ya Zari, watu mbalimbali mashuhuri wanatarajiwa kuhudhuria akiwemo dairekta mkubwa Afrika, Godfather wa Afrika Kusini na Top Ten ya Washiriki wa Shindano la Big Brother ‘Hot Shot’ 2014.

FANYA HAYA..!! UNAPOTOKEA KUMPENDA MTU ALIYE NA MPENZI WAKE






Tumshukuru Mwenyezi Mungu ambaye ametuwezesha kuonana tena wiki hii tukiwa wazima. Lakini pia tumshukuru kwa kutuletea kitu kinachoitwa mapenzi.
Mapenzi yamekuwa yakichukua nafasi kubwa sana katika maisha yetu ya kila siku na yamekuwa yakichangia kwa kiasi kikubwa furaha kwa kila mtu.
Kama huamini, angalia wale waliotokea kupenda na wao wakapendwa, utabaini nyuso zao zimetawaliwa na furaha isiyo na kifani. Lakini mapenzi hayo hayo yamekuwa ni chanzo cha vilio kwa baadhi ya watu.
Mpenzi msomaji wangu, kupenda hakuna macho! Moyo ukishapenda hausikii la kuambiwa. Katika hili ndiyo maana unaweza kumuona mwanaume kazimika kwa demu ambaye hawaendani kabisa lakini moyo wake ndiyo umeshapenda.
Ilishawahi kutokea msichana akampenda kijana mmoja ambaye ni fukara kupita maelezo. Yeye akawa ndiyo anamhudumia kwa kila kitu. Akamfanyia mpango wa ajira na mwisho wake wakafunga ndoa.
Sasa hivi wanaishi maisha ya furaha na amani. Wamegeuka mfano wa kuigwa kwa jinsi wanavyopendana lakini huko nyuma msichana huyo alikuwa akichekwa kwa kutoa penzi kwa mwanaume asiye na mbele wala nyuma.
Hayo ndiyo mapenzi jamani! Lakini pia katika kufurukuta kumtafuta mpenzi wa kuwa naye maishani, mwanaume anaweza kujikuta unaangukia kwa demu ambaye tayari ana mpenzi wake.
Moyo wako unakuambia yeye ndiye mtu sahihi katika maisha yako lakini tayari ana mtu wake, unafanyaje?
Utapambana kuhakikisha unapata kile ambacho moyo wako umekipenda au utakubaliana na ukweli kwamba huwezi kuwa naye kwa kuwa ana mtu wake? Inapofikia hatua hiyo unaweza kujikuta upo njia panda hasa pale ambapo huyo mwenye mtu wake naye anaonesha kuwa na chembechembe za mapenzi kwako. Kuna mambo kadhaa ya kukusaidia kukabiliana na hali hii.
Chunguza Tumia muda wako mwingi kuchunguza juu ya uhusiano wake. Uhusiano wao umesimama na wanaonekana ni watu wenye ‘future’? Nasema hivyo kwa sababu, yawezekana uhusiano wa huyo uliyetokea kumpenda ni wa kuzuga tu na huenda wewe ndiye mwenye ‘future’ naye. Ndiyo maana nikasema chunguza uhusiano wake kwanza.
Usitafute uadui Baada ya kuchunguza, ukibaini kwamba uhusiano wao hauko ‘siriasi’, vuta subira, lolote linaweza kutokea na likaufurahisha moyo wako. Lakini kama utaona ni watu walio siriasi na wanaelekea kuoana, usitafute uadui bure, kaa pembeni.
Una nafasi kwake? Sawa umetokea kumpenda msichana aliye na mtu wake, umeshawahi kujiuliza kama una nafasi ndani ya moyo wake? Anaonesha dalili fulani za kukupenda kama unavyompenda na ni mtu anayeonesha kukumisi anapokuwa mbali na wewe? Utakapobaini una nafasi kwake, uamuzi wa kumpotezea hautakuwa na nafasi.
Ni rahisi kubadili uamuzi wake? Unadhani huyo uliyetokea kumpenda anaweza kubadili maamuzi ya kumuacha huyo aliyenaye kama kweli hawana ‘future’? Utagundua hilo kwa kuongea naye na kumsikia kama anaweza kufanya maamuzi hayo ili awe na wewe.
Pingana na moyo wako Ifike wakati upingane na moyo wako. Unajua moyo wako kukuambia kuwa unataka kuwa na uhusiano na demu ambaye tayari ana mpenzi wake wakati mwingine utakuwa unakupotosha.
Kwa hiyo ukiona vipi, pingana nao. Acha kumng’ang’ania msichana mwenye mpenzi wake licha ya ukweli kwamba, huenda wewe ndiye mwenye nafasi ya kuwa mume wake na siyo huyo aliye naye.
Urafiki ni poa? Umempenda sana na hauko tayari kumkosa katika maisha yako lakini imetokea kwamba tayari yuko na mtu na umebaini huna nafasi kwake kabisa? Usiumie, omba angalau urafiki. Siyo urafiki wa kivile sana ila angalau pale unapotaka kusikia sauti yake kwa kumsalimia tu, upate nafasi hiyo.
Usiumie, yupo mwingine Haina haja ya kujitafutia vidonda vya tumbo bure kwa kuwa tu umebaini uliyetokea kumpenda tayari ana mtu. Chukulia ni hali ya kawaida, mademu wazuri ambao wanaishi singo wapo kibao huko mtaani, ni suala la wewe kutulia tu. Amini yupo mwingine ambaye atayafanya maisha yako yawe ya furaha.
Naomba nihitimishe kwa kusema kwamba, unapotokea kumpenda mtu fulani, pambana kuhakikisha unampata kwa sababu ukimkosa maisha yako yanaweza kuwa gizani. Ila pale utakapoona uwezekano wa kuwa naye haupo, usilazimishe ndugu yangu. Kumbuka haya ni maisha tu!

UKATILI ULIOJE! WAZAZI WAMPIGA, WAMFUNGA KAMBA MTOTO WAO, WAMFUNGIA NDANI


Katika hali inayoonyesha ukatili wa ajabu, mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Asha Mohamed, akishirikiana na mumewe, walimfunga kamba miguu na mikono mwanaye wa kumzaa Salum Mohamed (9) na kumfungia ndani ya nyumba yake huku wenyewe wakienda kusikojulikana muda mrefu Jumatatu iliyopita huko Mkundi, nje kidogo ya mji wa Morogoro.

Polisi wakimfungua kamba mtoto huyo alizokua amefungwa na wazazi wake.

Tukio hilo la kusikitisha lilifanyika ikiwa ni adhabu ya mtoto huyo kutokana kosa la kuchana chandarua kwa miguu, kitendo alichokifanya usiku wa Jumapili, ambako licha ya kupigwa kwa zaidi ya saa mbili mfululizo, pia alinyimwa chakula na hivyo kulala na njaa.

Polisi wakiwa wamembeba mtoto huyo.

Kwa mujibu wa majirani, Asha na mumewe ambaye ni baba wa kambo wa mtoto huyo, wamekuwa na tabia ya kumtesa, kitendo ambacho awali, kiliwahi kumfanya atoroke nyumbani hapo kukimbilia mjini kwa bibi yake, umbali wa zaidi ya kilomita kumi

Mama mzazi wa mtoto huyo aliefahamika kwa jina la Asha Mohamedi.

Kwa mujibu wa majirani Mwanamke huyo na mumewe kwa muda mrefu walikuwa wakimfanyia vitendo vya kikatili mtoto huyo”kuna wakati mtoto huyu aliamua kutembea kwa kwa miguu kutoka hapa mkundi mpaka mjini kwa bibi yake umbali wa kilomita 10.

Waandishi wa habari wakifanya mahojiano na mtoto huyo baada ya kufunguliwa kamba.

“Wazazi wake jana majira ya saa 3 mpaka saa 5 usiku walimpiga sana huyu mtoto, cha ajabu asubuhi walimfunga kamba na kumfungia kwa nje na kufuli kubwa na wenyewe kwenda kwenye shughuli zao, alishindwa kwenda shule, tulipomuuliza kupitia dirishani, alisema alipewa adhabu hiyo baada ya kuchana chandarua, kwa uchungu tukaamua kutoa taarifa kwako,” alisema Mage Luzimamu, mmoja wa majirani.

Baada ya mwandishi kupata taarifa hizo aliwasiliana na Jeshi la Polisi ambapo askari walienda hadi ilipo nyumba hiyo na kulazimika kuvunja mlango na baadaye kumfungua mtoto huyo na kuondoka naye. Mama mzazi alipatikana na kukiri kuhusika na tukio hilo, ambapo alijitetea kuwa alimfunga kamba kama sehemu ya adhabu na siyo mateso.

Mume wa mama huyo alikimbia baada ya kusikia taarifa za kusakwa kwake lakini Polisi wamesema watamtafuta hadi wamtie mbaroni.
Newer Posts Older Posts
© Copyright Bongo Mirror | Designed By BONGOJAMII.COM
Back To Top