Loading...

Mazishi ya baba yao wa P-Square

CHENGE AGEUKA MBOGO BUNGENI BAADA YA KUITWA FISADI...AMTAKA HALIMA MDEE ATOE USHAHIDI KUTHIBITISHA KAULI YAKE


MBUNGE wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) ametakiwa kuwasilisha ushahidi kuthibitisha kauli yake ya kumtuhumu Mbunge Bariadi Magharibi, Andrew Chenge (CCM), kwa ufisadi.

Chenge alilazimika kuomba utaratibu wa kiti juzi, baada ya Mbunge huyo wa Kawe kumtaja mara mbili wakati akichangia mjadala wa taarifa za kudumu za Bunge zilizowasilishwa juzi.




Mara ya kwanza, Mdee alimhusisha Chenge na mkataba mbovu wa Kampuni ya Ndege (ATCL) uliosababisha Serikali kuingia hasara ya zaidi ya Sh bilioni 90.

Licha ya kumtaja kwenye ufisadi huo ambao kwa mujibu wa Mdee, Chenge ndiye alikuwa Waziri wa Wizara yenye dhamana na ATCL, pia alimtaja kuhusika katika kashfa nyinginezo ikiwemo suala la utoaji takribani Sh bilioni 200, katika iliyokuwa Akaunti ya Tegeta Escrow ya Benki Kuu (BoT).

“Wabunge tuanze kuchunguzana humu ndani na kushughulikiana,” alisema Mdee na kutaja kwamba kwa kuanza, waanze na Chenge pamoja na Dk Shukuru Kawambwa (Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi), akimhusisha kuwa aliwahi kushika wizara hiyo yenye dhamana na ATCL.

Kauli hiyo ilimfanya Chenge kusimama na kusema; “kwa heshima zote nimemvumilia sana mheshimiwa (Mdee) anayechangia hoja hii. Kama ana ushahidi wa hayo anayosema, kanuni zetu zinatutaka ayawasilishe mbele yako.

“Mimi ningelipenda Bunge hili liendelee kuwa na heshima yake. Pili naomba sana, hayo wanayoyasema wawe na ujasiri wa kwenda kuyasemea nje ya ukumbi huu wa Bunge, wasijifiche kwenye kinga ya Bunge.

“Nina mengi ya kusema, lakini kwa sababu nimesimama kwa hoja ya utaratibu, kunitaja moja kwa moja, naomba aweke hoja mezani,” alisema Chenge.

Mwenyekiti wa Bunge alikubaliana kwamba Mdee awasilishe ushahidi kwa kiti. Hata hivyo Mdee alijibu, “Kuna utaratibu wa kikanuni, vielelezo nikitakiwa kuleta nitaleta.

"Tunazungumza hapa matumizi mabovu, mikataba mibovu na wizi wa mali ya umma. Mzee wangu (Chenge) ni rafiki yangu lakini nimeamua nimfungukie kwa sababu haya ni mambo makubwa.”

P-SQUARE KUMZIKA BABA YAO KESHO IJUMAA BAADA YA KUFARIKI MIEZI MIWILI ILIYOPITA!



Mzee Moses Okoye na mtoto wake Peter wa P Square. Hii ilikuwa siku ya harusi ya Peter.



November 26, 2014 taarifa kubwa kutoka Nigeria ilikuwa ni taarifa ya msiba wa mzee Moses Okoye, baba mzazi wa mastaa wa muziki kutoka Nigeria, P Square.



Tangu mzee huyo afariki ni miezi miwili sasa, yamepita matukio mengi huenda tukawa tumeanza kusahau tukio hilo, story iliyoko mitandaoni kutoka Nigeria ni kuhusu ndugu pamoja na familia ya mzee huyo kuandaa mazishi yake.

Tarehe ambayo imepangwa kufanyika mazishi hayo ni January 30, ambayo ni kesho siku ya Ijumaa.

AJALI YA MOTO KICHANGA CHAOKOA FAMILIA!

KICHANGA kinachokadiriwa kuwa na umri wa miezi nane, wiki iliyopita kiliiokoa familia yake kuteketea kwa moto, baada ya kuamka usiku na kulilia kunyonya, kitendo kilichomshtua mama yake aliyebaini nyumba yao ilikuwa ikiungua, huko Kibamba Lungwe jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya nyumba iliyoungua.
Akisimulia tukio hilo, mama wa kichanga hicho, Asha Mohamed, alisema alishtuka baada ya mtoto kuanza kulia akitaka kunyonya, alipoamka ndipo akaona mwanga mkali juu ya paa, hali iliyomlazimu kuamka na kwenda kumgongea Abuu ili kutafuta njia ya kutoka,” alisema mama huyo akiongeza kuwa sebuleni, moto ulikuwa umetapakaa.

Kijana Abuu Masoud (15), baada ya kuamshwa, alionyesha ujasiri na upendo mkubwa kwa kujitoa mhanga kuwasaidia wadogo zake watatu waliokuwa wamelala katika moja ya vyumba vya nyumba hiyo.
Baada ya kuingia katika chumba hicho, alifanikiwa kumtoa mtoto mmoja.
Watoto walionusulika kuteketea kwa moto.
“Nilipofungua mlango wa sebuleni nikaona moto na moshi mwingi sana, roho iliniuma sana kwani chumba cha pili kulikuwa na wadogo zangu watatu wamelala, nikaamua kuvaa ujasiri na kujitosa katika chumba kile na kufanikiwa kutoka na mtoto mmoja, wakabaki wawili,
baada ya kurudi ndani nikapata wazo la kuzima Mean switch, nilipoenda kuishika ikaniangukia kichwani kwani ilikuwa imeshaungua, ndiyo nikaungua na kushindwa kuwatoa waliobakia, ingawa baadaye kuna msamaria mwema mmoja alijitokeza na kuja kubomoa mlango na kuwatoa wengine,” alisema kijana huyo.
....Kitanda walichokuwa wamelala.
Mama wa mtoto mchanga alifanikiwa kutoka pasipo kudhurika.
Aidha baba mwenye nyumba hiyo, Khalfani Maketemo, ambaye wakati nyumba yake inaungua yeye na mkewe walikuwa hospitali alikokuwa amelazwa, anadai chanzo cha moto huo ni shoti iliyoanzia kwenye bati na anaamini ni kutokana na kuunganishwa vibaya kwa waya unaopitisha umeme kutoka kwenye nguzo kwenda kwenye nyumba.
Wakizungumza na mwandishi wetu baadhi ya majirani walisema; “Uunganishwaji wa umeme ni wa kubabaisha, waya unagusana na bati jambo ambalo ni hatari kama waya utachubuka na mvua kunyesha’’.Familia hiyo kwa sasa haina sehemu ya kujisitiri nyumba nzima imeteketea.

KIJANA AUAWA NA KUTELEKEZWA KARIBU NA KAMBI YA FFU







Kijana ambaye hakufahamika jina anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 30 hadi 35 amekutwa ameuawa na mwili wake kutelekezwa katika eneo la kambi ya Polisi Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) kata ya Nshambya mkoani Kagera.


Mwili huo uligundulika majira ya saa sita mchana baada ya watu waliopita katika eneo hilo kuuona ukiwa umelazwa karibu na moja ya shamba lililopo mtaa wa Bunkango eneo la kambi hiyo ya Polisi.


Mpekuzi ilishuhudia mwili huo ulioanza kuharibika ukiwa umevuliwa nguo zote ukiwa bado haujaondolewa katika eneo hilo la tukio.

Mwili huo ulikuwa na majeraha maeneo ya usoni kiasi cha kushindwa kutambulika kirahisi.

Akizungumza na waandishi wa habari waliofika katika eneo hilo, Kaimu Mtendaji wa kata ya Nshambya, Christian Ngaiza, alisema alipata taarifa za tukio hilo kutoka kwa dereva wa bodaboda kuwa kuna mtu ameuawa lakini wananchi wanaogopa kutoa taarifa Polisi.


Ngaiza, alisema baada ya kupata taarifa hiyo aliamua kwenda eneo la tukio majira ya saa saba mchana na kutoa taarifa ya tukio hilo Polisi.

Aidha, alisema baada ya kubaini mwili huo, alianza uchunguzi na kuhoji wananchi wa mitaa yote mitatu ya eneo hilo endapo wana taarifa za mtu yeyote aliyepotea ambapo ilibainika hakukuwa na mtu aliyepotea.

Mkazi wa Mtaa wa Migera, Joyce Nuru, akizungumzia tukio hilo, alisema alipata taarifa za kukutwa kwa maiti huyo, akiwa nyumbani kwake ambapo majira ya saa sita mchana wanafunzi walipita na kumueleza kuwa kuna mtu amekufa maeneo ya mnara.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera ambaye pia ni mpelelezi wa makosa ya jinai mkoani humo, Gilles Mroto alisema tukio hilo amelisikia na ametuma timu ya maofisa wa Polisi kwenda eneo la tukio kufanya uchunguzi.

Hata hivyo, mwili huo haukuweza kutambulika na hivyo kuzikwa na Manispaa ya Bukoba katika makaburi ya Kyebitembe

cr : Jamvi la Habari Tanzania

Kaseja kupandishwa tena kizimbani february 22



Kipa wa Yanga, Juma Kaseja kupitia kwa wakili wake, Samson Mbamba, jana amesomewa shtaka lake kwa mara ya kwanza la kuvunja mkataba kwenye Mahakama ya Kazi.

Kesi hiyo itaunguruma tena Februari 12 na Yanga wanataka Kaseja awalipe Sh340 milioni ikiwa ni ada ya usajili, ambayo ni Sh40 milioni pamoja na fidia ya Sh300 milioni, ambazo ni gharama za usumbufu wa kuvunja mkataba, kumhudumia na kutunza kiwango chake kwa kipindi chote alichokuwa Yanga.

Yanga inawakilishwa na mwanasheria wao, Frank Chacha, ambaye alifungua kesi hiyo Ijumaa iliyopita na ameliambia gazeti hili kuwa wamefikia uamuzi huo ili iwe fundisho kwa wachezaji wengine kuheshimu mikataba yao.

Kaseja aliingia kwenye mgogoro na uongozi wa Yanga baada ya Novemba 11 mwaka jana, kuandika barua ya kuvunja mkataba na klabu hiyo baada ya kukiuka makubaliano ya mkataba kati yao, akishinikiza kulipwa Sh20 milioni za usajili alizokuwa anaidai klabu hiyo.

Kaseja kupitia Kampuni ya Mbamba Advocate, iliandika barua ya kuvunja mkataba na klabu hiyo kwa kile ilichoeleza kuwa amekuwa akisugua benchi.

Pia, uongozi wa Yanga umekiuka makubaliano baina ya pande mbili ambazo hadi Januari mwaka jana walitakiwa kummalizia ada yake ya usajili Sh20 milioni, lakini hata hivyo, haikufanya hivyo hadi alipowasilisha barua ya kuvunja mkataba.

Akizungumza na gazeti hili, Wakili wa Kaseja, Samson Mbamba alisema: “Tutasimama kizimbani, hakuna shida, wala hatubabaishwi na lolote, naamini mteja wangu ana haki zote, mbivu na mbichi zitajulikana.”

Kwa upande wake, kipa huyo wa zamani wa Simba, Kaseja, alisema hana la kusema kwa sasa na kila kitu amekiacha mikononi mwa wakili wake

Kipa wa Yanga, Juma Kaseja kupitia kwa wakili wake, Samson Mbamba, jana amesomewa shtaka lake kwa mara ya kwanza la kuvunja mkataba kwenye Mahakama ya Kazi.

Kesi hiyo itaunguruma tena Februari 12 na Yanga wanataka Kaseja awalipe Sh340 milioni ikiwa ni ada ya usajili, ambayo ni Sh40 milioni pamoja na fidia ya Sh300 milioni, ambazo ni gharama za usumbufu wa kuvunja mkataba, kumhudumia na kutunza kiwango chake kwa kipindi chote alichokuwa Yanga.

Yanga inawakilishwa na mwanasheria wao, Frank Chacha, ambaye alifungua kesi hiyo Ijumaa iliyopita na ameliambia gazeti hili kuwa wamefikia uamuzi huo ili iwe fundisho kwa wachezaji wengine kuheshimu mikataba yao.

Kaseja aliingia kwenye mgogoro na uongozi wa Yanga baada ya Novemba 11 mwaka jana, kuandika barua ya kuvunja mkataba na klabu hiyo baada ya kukiuka makubaliano ya mkataba kati yao, akishinikiza kulipwa Sh20 milioni za usajili alizokuwa anaidai klabu hiyo.

Kaseja kupitia Kampuni ya Mbamba Advocate, iliandika barua ya kuvunja mkataba na klabu hiyo kwa kile ilichoeleza kuwa amekuwa akisugua benchi.

Pia, uongozi wa Yanga umekiuka makubaliano baina ya pande mbili ambazo hadi Januari mwaka jana walitakiwa kummalizia ada yake ya usajili Sh20 milioni, lakini hata hivyo, haikufanya hivyo hadi alipowasilisha barua ya kuvunja mkataba.

Akizungumza na gazeti hili, Wakili wa Kaseja, Samson Mbamba alisema: “Tutasimama kizimbani, hakuna shida, wala hatubabaishwi na lolote, naamini mteja wangu ana haki zote, mbivu na mbichi zitajulikana.”

Kwa upande wake, kipa huyo wa zamani wa Simba, Kaseja, alisema hana la kusema kwa sasa na kila kitu amekiacha mikononi mwa wakili wake

YANGA KUMPANDISHA KIZIMBANI JUMA KASEJA



Baada ya Uongozi wa Klabu ya Yanga kutangaza kuachana na aliekuwa mlindamlango wake Juma Kaseja na baadae kumfungulia mashtaka katika Mahakama ya kazi , hatimaye mlind amlango huyo sasa anatarajia kusomewa mashtaka yanayomkabili February 12 mwaka huu.
Hatua hiyo ilikuja kufuatia Kaseja kudai alipwe fedha zake za usajili zilizokuwa zimesalia na kutaka kuvunja mkataba wake , lakini baadae Klabu hiyo ilimuingizia pesa hizo katika akaunti yake bila kumpa taarifa na kupelekea kuwepo kwa mgogoro baina ya pande hizo mbili.
Mkuu wa Idara ya Sheria ya Klabu hiyo FRANK CHACHA ameiambia mtandao huu kwamba wamepokea samasi inayomtaka mlindamlango huyo kufika Mahakamani hapo kwa ajili ya kesi hiyo

YULE MAMA MWENYE MAPACHA 6 ALIYEKIMBIWA NA MME ETI KISA ANAZAA SANA APATIWA NYUMBA NA COVENANT BANK



Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Covenant Bank Balozi, Salome Sijaona(Katikati) akikata utepe, kuashiria uzinduzi Rasmi wa nyumba aliyokabidhiwa Salome Mhando ambaye alitelekezwa na mume wake baada ya kujifungua watoto mapacha mfurulizo hadi kufikia sita na kukosa Mahali pa kuishi, Covenant Bank imemkabidhi nyumba hiyo ambayo ataimiliki yeye mwenyewe pamoja na thamani za ndani na Bima ya Matibabu kwa Mwaka mzima. Anaeshuhudia ni mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Sabetha Mwambenja (wa kwanza kushoto) na Salome Mhando (wa kwanza kulia).




Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Covenant Bank Balozi, Salome Sijaona (kushoto), Pamoja na Mkurugenzi wa benki Hiyo, Sabetha Mwambenja, wakimkabidhi hati ya kiwanja na Umiliki wa nyumba Salome Mhando, Mama alietelekezwa na mume wake baada ya kujifungua watoto mapacha mfurulizo, hadi kufikia sita, Benki hiyo imemkabidhi nyumba hiyo pamoja na Bima ya Matibabu kwa mwaka mzima.




Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Covenant Bank Balozi, Salome Sijaona(Katikati) akiwapokea watoto wa Salome Mhando wakati akiwasili kukabidhiwa nyumba yake. Pamoja nae ni Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja na Mjumbe wa Bodi ya benki hiyo, Margaret Kyarwenda.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Covenant Bank Balozi, Salome Sijaona (wa kwanza kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja na Mama Salome Sijaona, Wakimfurahia moja wa watoto wa mama huyo akipanda katika moja ya vitanda walivyokabidhiwa.





Baada ya kujifungua watoto mapacha mfululizo na kufuatiwa na kitendo cha kutelekezwa na mume wake huku akiwa hana sehemu ya kuishi, Hatimaye Salome Muhando amenunuliwa na kukabidhiwa nyumba na Covenant Bank ambayo ataishi yeye na watoto wake.



Salome , mwenye watoto sita mapacha alitelekezwa na mume wake baada ya kujifungua mapacha mara tatu mfululizo na kusababisha kukosa sehemu maalum ya kukaa yeye pamoja na watoto wake ambapo baada ya kutelekezwa msamaria mwema alijitolea kumhifadhi katika shamba lake lililopo eneo la Mabwepande.



Baada ya kusikia kilio cha mama huyo kupitia vyombo vya habari Covenant Bank, ilijitolea kumnunulia nyumba mama huyo ambayo ataimiliki yeye moja kwa moja na kumpatia mtaji wa biashara ambao utamsaidia kuenesha maisha yake ya kila siku.



Akizungumza na waandishi wa habari, punde baada ya kukabidhi nyumba hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo Balozi, Salome Sijaona, amesema baada ya kuona mateso ambayo mwanamke huyo amekuwa akiyapata kwa kukosa makazi , Chakula na mahitaji mengine ya kibinaadamu waliona ni vyema benki yake kujitolea kumsaidia ikiwa ni katika sehemu moja ya kutimiza majukumu yake ndani ya jamii.



“Tumeguswa sana na mateso ambayo amekuwa akiyapata Bi. Salome Mhando, yeye pamoja na watoto wake baada ya kutelekezwa na mume wake kwa kigezo ha kuzaa watoto mapacha mfurulizo, tuliguswa na kuamua kujitolea kumnunulia nyumba ambayo ataimiliki yeye mwenyewe.” Alisema Balozi, Sijaona na kuongeza kuwa.



“Nyumba hii tumemkabidhi pamoja na samani za ndani ya nyumba ambazo zitamuwezesha sasa kuishi maisha ya amani, na furaha akiwa kama wanawake wengine na kufurahi pamoja na watoto wake.”



Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Sabetha Mwambenja amesema kuwa pamoja na kumkabidhi nyumba mama huyo pia Benki hiyo, imempatia Bima ya Matibabu kutoka AAR ambayo itamsaidia kupata Matibabu yeye pamoja na watoto wake wote.



“Pamoja na kumpatia nyumba Salome pia tunampatia Bima ya Matibabu ambayo itamuwezesha yeye na watoto wote kutibiwa katiba Hopitali zote zilizo mahali popote nchini, Tuna uhakika sasa atakuwa na uhakika wa afya yake na watoto wake katika kipindi chote hivyo atakuwa na nafasi ya kufanya shughuli zake za uzalishaji kwa amani., Alisema Mkurugenzi huyo.



Kwa Upande wake Salome , aliwashukuru Covenant Bank kwa kujitolea kumsaidia na sasa ana uhakika wa maisha yeye pamoja na watoto wake.



“Ninawashukuru sana Benki ya Covenant kuniwezesha kumiliki nyumba yangu ninawashukuru sana na ninaomba waendelee na moyo huo wa kuwasaidia kina mama wenye matatizo kama haya kwa sababu siko peke yangu,” alisema na kuongeza,




“Kina mama tumekuwa na wakati mgumu sana katika ndoa zetu hususai katika masuala ya uzazi, Ninawashukuru watu wote ambao walijitolea kunisaidia chakula na nguo katika wakati wote ambao nilikuwa sina sehemu maalum ya kukaa, hadi sasa ninamiliki nyumba yangu. Alihitimisha Salome
Newer Posts
© Copyright Bongo Mirror | Designed By BONGOJAMII.COM
Back To Top